Mchezaji Tshishimbi, Yanga Kimeeleweka


HATIMAYE kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi amevunja ukimya wa muda mrefu na kusema kwamba, kesho Jumatatu anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo.

Hilo limekuja ikiwa ni miezi michache kupita tangu zienee Tshishimbi, Yanga kimeelewekar taarifa za kiungo huyo kugoma kuongeza mkataba na kuingia kwenye rada za Simba.

Tshishimbi anaongeza mkataba huo mara baada ya uongozi wa Yanga kumpa kile alichokuwa anakihitaji ikiwemo kumuhakikishia kuwa timu hiyo inakwenda kufanya usajili ambao utaifanya Yanga kuwa tishio.
 
Akizungumza na Spoti Xtra, Tshishimbi alisema kila kitu kuhusu kuongeza mkataba huo kimekwenda vizuri, viongozi wamekubali kumtimizia mahitaji yake na yeye ameona ni bora aendelee kuwepo Yanga kutokana na uwepo wa mipango mizuri ya kukiboresha kikosi hicho kwa msimu ujao ambayo inafanywa na uongozi.

 
“Kila kitu kipo vizuri na nimezungumza na uongozi tumekubaliana, muda wowote kuanzia sasa nitasaini mkataba mpya kwa sababu viongozi wameniambia msimu ujao mambo yatakuwa mazuri,” alisema Tshishimbi.

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alitia mkazo ishu hiyo kwa kusema: “Nadhani mmemsikia mwenyewe akizungumza hapo, kwa hiyo manenomaneno kayamaliza. Si amesema ndani ya siku mbilli hizi atasaini, basi mimi nawaambia huenda Jumatatu mambo yote yakawa vizuri.”

STORI: ISSA LIPONDA, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad