Katibu mkuu wa baraza la habari nchini (MCT) Kajubi Mukajanga ametoa sababu kadhaa za kutaka wanahabari waliojitokeza kugombea kwenye vyama mbalimbali vya siasa nchini kuacha kufanya kazi za habari.
Akinukuliwa na mtandao wa millardayo.com Katibu wa MCT amesema baraza hilo halina mamlaka ya kumfukuza muajiliwa ila litafanya mazungunzo wajiri ili kulinda maadili ya kazi ya uandishi wa habari.
“Mwandishi akitaka kugombea anatakiwa aache kazi kwanza, akigombea katika Chama fulani na akaendelea na kazi yake ya habari, sisi Baraza la Habari tunazungumza na mwajiri wake, kwasababu sisi sio Waajiri tunasimamia maadili, akibaki kazini ataonekana kama kada”amesema Kajubi.
Mapema Julai 22,2020 Baraza la haabri nchini (MCT) lilitoa walaka wa kutaka wanahabri wote waliojitkeza kugombea kwenye vyama vya siasa kuacha kazi kutoka na mgongano w akimaslai na ukiukaji wa maadili ya kazi ya uwandishi wa habari.
“Kwanini hili linaonekana kama ni kitu cha ajabu, mantiki ile ile inayotumika kumkataza Mtumishi wa umma kushiriki siasa za ushindani wa vyama akiwa Mtumishi wa umma ndio mantiki hiyohiyo inayomzuia mwanahabari kushiriki siasa za ushindani akiwa ndani ya chumba cha habari"-KAJUBI pic.twitter.com/gLLOXdaLiS— millardayo (@millardayo) July 23, 2020