Meya Jacob: Dk. Ndugulile Tunaomba Namba ya Tigopesa Tuwatumie Pesa Wapiga Kura Kigamboni


Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, amemuomba mshindi wa kura za maoni jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile ampatie namba ya tigopesa au Mpesa ili kuwatumia fedha wapiga kura Kigamboni.

Jacob alisema lengo la kutuma fedha hizo ni kutaka kuwapatia walau soda kwa kazi nzito waliyoifanya jana.

Jacob aliandika ujumbe huo jana katika ukurasa wake wa twitter baada ya kutangazwa kwa matokeo katika uchaguzi wa kura za maoni kwa wagombea wa jimbo la Kigamboni.

Katika matokeo hayo Dk. Faustine Ndugulile alipata ushindi wa kura 190 sawa na asilimia 45 na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipata kura 122 sawa na asilimia 30.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad