Miili ya watu 7 imegunduliwa katika kaburi moja katika mji uliokuwa umetekwa na waasi Libya.
Miili ya watu 7 ambao wanakisiwa kuwa raia imegunduliwa katika mji wa Terhune , mji ambao ulikuwa imetekwa na waasi nchini Libya.
Mji huo ulikombolewa mnao Juni 5 baada ya makabiliano makali kati ya jeshi la serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa na wapiganaji wa jenerali Khalifa Haftar.
Kiongozi wa jopo lililoandaliwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji katika maeneo yaliokuwa yametekwa na waasi lÄ°BYA Kemal es Seyewi amefahamisha kuwa katika hatua iliopigwa hadi kufikia sasa ni miili ya watu 7 ndio iliogunduliwa katika kaburi la pamoja.
Miili hiyo imepelekwa katika hospitali moja ili ihifadhiwe na kuzikwa kwa heshima.
Kulingana na taarifa zilizotolewa na serikali hiyo inayotambulika na jumuiya ya kimataifa, Terhune kuna zaidi ya makuburi 11 ya pamoja.
Wapiganaji wa Haftar waliondoka katika eneo hilo baada ya kuzidiwa na mashambulizii yalioendeshwa kwa ushirikiano na jeshi la Uturuki.