Zitto ametangaza maamuzi hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter leo Julai 25, 2020 na kusema chama hicho kinaendelea kutoa pole kwa familia ya Mkapa na taifa kwa ujumla.
“Tumeahirisha shughuli yetu ya kisiasa Leo ya Wananchi wa Lindi kumkaribisha Bernard Membe nyumbani ili kupisha shughuli za maombolezo ya Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa. Tunaendelea kuwapa pole Watanzania na Famiia ya Rais Mkapa kwa msiba mzito huu. Maisha ya Mkapa kiuongozi ni Mafunzo” ameandika Zitto.
Rais Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Julai 24,2020 akiwa hospitali jijini Dar es salaam alikikuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano julai 29,2020 Mkoani Mtwara.
Mimi na Familia yangu tumestushwa na kusikitishwa sana na kifo cha ghafla cha Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa. Tutamkumbuka kwa akili kubwa ya uchambuzi, Uwezo wake wa kusuluhisha migogoro barani Afrika, na Uwanadiplomasia uliotukuka. Poleni wanafamilia.RIP- BMW.— Bernard K. Membe (@BenMembe) July 24, 2020