Mobeto Hataki Kabisa Ushauri Penzini


MWANAMITINDO maarufu na mwanamuziki Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka kuwa, kamwe hawezi kumshauri mtu yeyote mahusiano yake ya kimapenzi, kwani mapenzi hayashauriwi.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema katika mambo ya uhusiano wa kimapenzi, ni vigumu kumshauri mtu hata siku moja kwa sababu hata yeye alivyokuwa kwenye mapenzi, walijitokeza watu mbalimbali na walimshauri sana, lakini hakuwaelewa kabisa, akaendelea na mambo yake.

“Kwenye mapenzi siwezi kumshauri mtu yeyote hata rafiki wangu wa damu, maana ni jambo gumu kumwambia mtu akakuelewa, ni vizuri kila mtu akajiongoza mwenyewe,” alisema Mobeto

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad