Morrison Alidanganya Asingecheza Bila Mkataba.



Kamati ya katiba,sheria na hadhi za wachezaji ya TFF imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi bila ya kuwa na mkataba,hivyo kauli ya Benard Morrison kuwa alicheza mechi mbili mbila mkataba ni uongo

Kamati ya katiba,sheria na hadhi ya wachezaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi kuu bila ya kuwa na mkataba.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo,Elius Mwanjala ametoa kauli hiyo akitolea ufafanuzi alichokisema mchezaji Benard Morrison kuwa aliitumikia Yanga katika michezo miwili bila ya kuwa na mkataba.

Mwanjala amesema kauli ya Benard Morrison ni ya uongo kwa kuwa utaratibu wa wachezaji wote kucheza ligi kuu unafahamika ni lazima awe na mkataba ili kupata usajili na uhalali wa kucheza ligi kuu.

Kuhusu masuala mkataba wa Morrison ,Mwanjala amesema wanasubiri kupokea baadha ya nyaraka kutoka Yanga ili kufahamu ulalali wa mkataba wa miaka miwili ambao mchezaji anakana kuwa hajausaini.

Hata hivyo kamati hiyo imekiri kuipokea mikataba ya miezi sita na miaka miwili ya mchezaji huyo lakini wanasubiri kikao cha mwisho kuzipitia nyaraka zitakazowasilishwa na Yanga.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema wanaendelea kushughulikia malalamiko ya Yanga ambao waliyafikisha katika kamati yao juu ya moja ya klabu nchini kutumika kumrubuni mchezaji wao Benard Morrison kiasi cha kuukana mkataba wao.

Vile vile kamati imesema itatoa hukumu ya pamoja dhidi ya makamu mwenyekiti wa Yanga,Fredrick Mwakalebela ambaye amelalamikiwa kuleta taharuki ndani ya wekundu wa msimbazi kwa kutangaza katika vyombo vya habari kuwa wamekamilisha mazungumzo na kiungo wao Clautus Chama kinyume na utaratibu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad