Mrembo Mpya wa Diamond, Mama Dangote Atoboa SIRI



Tukubali, tukatae!! Miongoni mwa mastaa bongo ambao wamefanikiwa kuteka hisia za mashabiki wengi wa burudani, Jina la Diamond Platnumz siku zote limekuwa halikosekani kwenye list! Mahusiano yake, kazi zake, familia yake na hata uwekezaji wake kwenye miradi mbalimbali na kusaidia watu vimekuwa ni vitu ambavyo vinamuweka kwenye ‘Peak’ kila siku.

Weekend iliyopita, tarehe 18 July, team nzima ya WCB waliandaa show bab kubwa ya kumtambulisha rasmi msanii mpya wa kike wa lebo hiyo, Zuhura Kopa maarufu kama Zuchu. Tukio hilo lilikuwa ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani hapa Bongo, na miongoni mwa matukio ya kihistoria katika TASNIA ya burudani ndani ya WCB na Tanzania kiujumla kwani lilifanikiwa kuteka ‘Atensheni’ ya wapenda burudani wote bongo. Mastaa wakubwa, wanasiasa na wapenda burudani wote Bongo macho yao yalikuwa kwenye show hiyo.. Na asikwambie Mtu, Show ilikuwa Bab kubwa!!

Katika Event hiyo watu walikuwa wana ‘expekti’ kumuona Diamond akiwa ameambatana na mwenza wake, ambaye kwa sasa ‘Hajulikani’ ni nani, Masaa machache kabla ya show kuanza Diamond Kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika

“Kama Unavyojua Red Carpet inahitaji wa Ubavu wa Kushoto, na Mie ndio Sina basi nisaidieni kunichagulia ata wa kuingia nae tu kwa RED CARPET ya #IAMZUCHU Mlimani CityLeo……”.

Baada ya post yake hiyo, Wadau wengi walihisi kuna ‘Sapraizi’ watakutana nayo pale huku wengi wakihisi kuwa Diamond ataingia ukumbini na Zari, ambaye kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na ukaribu mkubwa, jambo ambalo halikuwepo mwanzo. Kuthibitisha tetesi zile, Diamond aliwahi kuulizwa na waandishi kama Zari atakuwepo, na Diamond aliwajibu kwa kifupi ” Show hii ni kubwa, karibu kila mtu anatamani kuwepo, hivyo fans tegemeeni chochote….”



Lakini tofauti na ilivyotegemewa, Diamond alitinga ukumbini akiwa na msanii wake Zuchu kitendo ambacho kiliwakata ‘Maini’ watu waliotegemea kumuona akiwaa na bebi mama wake.


NDANI YA UKUMBI

Akiwa ndani Diamond alionyesha kuwa busy na event huku akiwa hayuko ‘attached’ kwa mwanamke yeyote, tofauti na Hamisa, Wema na wengine ambao alipata fursa ya kucheza nao mziki.

MAMA DANGOTE ATOBOA SIRI

Katika tukio hilo, kuna warembo kibao ambao walitokea wakiwa ‘wamewaka’ balaa na kupendezesha Red carpet ya tukio hilo. Lakini kitu ambacho kiliwaacha watu na maswali kibao ni kitendo cha mama yake mzazi Diamond, Mama Dangote kumpost mrembo mmoja tu zaidi ya mara moja katika ukurasa wake wa instagram na kutoweka caption yoyote!! Kitendo ambacho kiliwaaminisha watu kuwa huyo ndio ‘Mrithi wa Tanasha’.


Wafuatiliaji wa mambo walienda mbali zaidi na kulinganisha hadi nguo walizovaa Diamond Platnumz na mrembo huyo, ambaye anajulikana kama Jihan Dimack ambaye aliwahi kunyakua taji la Miss Universe mwaka 2016/2017. Moja ya comment kutoka katika post hiyo ilisomeka 
” Huyo ndio mkwe wako, watu wazima tushaelewa…maana hadi nguo wamevaa sare sare na Diamond”

Ukiachana na nguo, wadau waliendelea kutoa maoni yao kwenye post hizo alizoziweka ‘Mama Dangote’.
“Kati ya wooote, umemuona huyo tu? tushamjua shemeji wa taifa”



Comment nyingine kutoka kwa mdau wa Lebo ya WCB, ndio iliwaaminisha zaidi wananzengo

“Mimi mwanao🙌 najua na ninatambua malengo yk msimamo wako na ujawahi kufeli hata siku1 boss @mama_dangote wacha vijuso wajitekenye wenyewe kiama chao mwezi 8 au 9 💌


Wadau wa mambo ya ‘Ufukunyuku’ walienda mbele zaidi na kudai kuwa sio kawaida kwa Mama Dangote kupost picha za warembo kwenye matukio kama hayo, hasa hasa kwenye ukurasa wake wa instagram, hivyo kitendo cha kumpost Jihan zaidi ya mara moja, kinaashiria kuna Ukaribu kati yao, na ukaribu huo unaweza kuwa ni ukaribu wa ‘Mtu na mkwewe’.

STORY NA : CHASAMA JR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad