Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kama klabu hiyo imemchoka basi yupo tayari kujiuzulu nafasi yake kutokana na kupewa tuhuma za kuihujumu klabu hiyo.
Mwakalebela ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu tuhuma zinazomuhusisha kupanga mipango ya kuihujumu Yanga kuelekea katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Lipuli FC utakao chezwa uwanja wa samora mkoani Iringa.
Katibu huyo wa zamani wa TFF amenukuliwa akisema ‘leo kwa kweli nimesikitika sana mpaka naamua kusema maneno haya na naongea huku nikitoa machozi mimi nimekuwa nikisemwa maneno mengi, lakini naamua kukaa kimya ili kuleta amani na usalama’.
Kwa mujibu wa Mwakalebala anasema alikwenda mkoani Iringa kumuuguza mama yake ambae ni mgonnjwa lakini ameshangazwa baada ya kurejea Dare s salaam anaambiwa alikuwa anafanya mipango ya kuihujumu Yanga.
"Naambiwa leo Mwakalebela anahijumu Yanga timu inaenda hotel ambayo ni ya Lipuli jamani naomba kama tumechokana niache uongozi kwa kweli naomba niwachie kwa amani kila linalokuwa baya ni Mwakalebela hivi mimi nina nguvu gani kwenye Yanga kufanya hivyo?"
Uongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti Dr Mshindo Msola umekuwa ukitajwa kuwa na makando kando mengi ikiwemo viongozi wa klabu hiyo kutokuwa na maelewano baina yao.
Mnamo Mwezi Machi mwaka huu wajumbe watatu wa kamati ya utendaji walijiuzulu na wengine wawili walisimamishwa kwa kile kilichodaiwa kutokubaliana na baadhi ya mambo yanavyoendeshwa klabu hapo.