Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.
Amendika historia kwa kuwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha ''Wings of Glod'' au ''mbawa za dhahabu'', baadae mwezi huu wa Julai, kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa Alhamisi wiki hii na Mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi za majini.
Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi "BZ," au "Bravo Zulu,"neno linalotumiwa na wanajeshi -wanamaji , linalomaanisha "umefanya vyema."
"BZ kwa Lt. j.g. Madeline Swegle kwa kumaliza mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi (ya mashambulio) ya anga,"aliandika Mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini. "Swegle ni @Mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anayetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea Mbawa za dhabahabu baadae mwezi huu .
HOOYAH!", uliandikwa ujumbe wa mkuu huypo wa mafunzo.
Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kumsusu rubani huyu mpya, Swegle kwa sasa yuko katika kituo cha mafunzi cha Redhawks Squadron (VT) 21 katika kituo cha Ndege za vita vya majini -Naval Air Station cha Kingsville kilichopo Texas.
Picha ambazo ziliambatana na twitter ya kikosi cha majini ya kusherehekea mafanikio ya kihistoria ya Bi Swegle zilichukuliwa baada ya safari yake ya mwisho ya ndege ya Mkakati wa mashambulizi ya kivita.