Mwanamke Zimbabwe Apigania Mashine itengenezwe ili Asikate Matiti
0
July 13, 2020
Mwanamke wa miaka, 44, nchini Zimbabwe, Tendayi Gwata, inakabiliwa na tishio la kukatwa matiti baada ya matibabu yake ya saratani kukatizwa ghafla.
Hiyo ni baada ya mashine moja pekee ya tiba ya saratani ya njia ya miale ya 'radiotherapy' katika mji mkuu wa Harare, kuharibika.
Bi. Gwata ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mauzo tayari amepoteza nywele zake kichwani wakati akifanyiwa tiba ya chemotherapy.
Sasa ameambiwa huenda akakatwa matiti kwa sababu mashine imeharibika.
Sekta ya afya nchini Zimbabwe imeathiriwa pakubwa na kuzorota kwa uchumi ambako kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumko wa bei kwa hadi aslimia 785 na uhaba wa fedha.
Mdororo wa kiuchumi umekuwa mbaya zaidi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Mwezi Julai 2019 nilihisi maumivu kwenye titi langu nikaamua kwenda kumuona daktari mjini Harare ambapo nilifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Matokeo ya uchunguzi huo yalibaini naugua saratani ya matiti ambayo imesambaa hadi chini ya kwapa langu.
Tags