Mwanamuziki Rayvanny Azidi Kupaa...Ashirikishwa Kwenye Ngoma na DJ Cuppy, Rema Naye Ndani
0
July 22, 2020
STAA mwingine wa Bongo Fleva kutoka Usafini WCB, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye anatesa Afrika Mashariki, sasa ametisha kule Afrika Magharibi baada ya kupiga kolabo na mwanamuziki wa Nigeria, Cuppy.
Katika singo hiyo mpya inayokwenda kwa jina la Jollof On The Jet iliyoachiwa hewani kwa mara ya kwanza juzi Jumamosi, yupo mwanamuziki mwingine kutoka Nigeria, Rema ambaye naye ameonesha makali yake.
Jollof On The Jet ni ngoma yenye mirindimo ya Afro-Pop, ambayo kwa pamoja; wasanii Cuppy, Rayvanny na Rema wameutendea haki.
Akizungumzia kuhusu kolabo hiyo, Cuppy alisema; “Kiukweli mseto wangu na Rayvanny na Rema ni wa kipekee. Tumerekodi tukiwa mbalimbali, haikuwa rahisi kuwa pamoja studio. Kila mmoja alirekodi kivyake kisha kazi ya kuchanganya sauti ikafanywa studio. Naamini hii ni kazi bora kabisa.”
Makali ya Cuppy yalianza kudhihirika tangu mwaka 2014, alipochaguliwa kuwa DJ bora wa mwaka katika Tuzo za Muziki za MTV (MTV Africa Music Awards).
Ngoma nyingne za Cuppy zinavyotingisha ni Green Light akiwa na Tekno na Gelato akiwa na Zlatan.
Tags