Mwandishi Afungwa Miezi Sita kwa Kuikosoa Serikali Kuhusu Corona
0
July 29, 2020
Mahakama ya Somalia imemuhukumu miezi sita mwandishi wa habari maarufu nchini humo Abdiaziz Ahmed Gurbiye, mhariri mkuu na naibu mkurugenzi wa shirika binafsi la Goobjoog, mjini Mogadishu
Alishtakiwa kwa kuikosoa serikali ya Somalia katika kukabiliana na mlipuko wa corona.
Mahakama ya mjini Banadir ilimtaka kutoa faini ya shilingi milioni tano za Somalia (208.3 USD) kwa kuchapisha taarifa za kizushi na kuitusi serikali na mahakama, muda mfupi baada ya kuhamishiwa katika gereza la Mogadishu.
Wakili wake anasema mahakama ilitumia sheria iliyopitwa wakati kutoa hukumu hiyo.
Kesi ya Gurbiye imekuwa ikiendelea kwa miezi kadhaa, ilikuwa ni mongoni mwa kesi kubwa dhidi ya waandishi nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni.
Tags