Mwigizaji wa Ghana Aliyepiga Picha za Utupu na Mtoto Wake, Aomba radhi
0
July 02, 2020
Mwigizaji wa Ghana wa Rosemond Brown maarufu kama Akuapem Poloo ameomba radhi baada ya kupost picha ya utupu (kama alivyozaliwa) akiwa na mtoto wake wa miaka saba.
Akuapem Poloo alipost picha hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram Jumatatu, Juni 30, 2020 kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake aliyetimiza miaka saba.
Watu mbalimbali, vyombo vya habari, walimtuhumu mwigizaji huyo pamoja na mashirika kadhaa ya asasi za kiraia, na Shirika la Haki za watoto la Kimataifa kuitaka Idara ya Upelelezi wa Jinai ya Polisi (CID) ya Huduma ya Polisi ya Ghana kuangalia jambo hilo kuwa ni kama uvunjaji wa kanuni ya ustawi wa Sheria ya Mtoto.
Pamoja na kuomba msamaha alisema; Yeye huoga bafuni pamoja na mtoto wake huyo kila wakati.
Tags