Mwimbaji wa muziki Remmy Ongala ni mzaliwa wa Februari 10 1947 ambaye Desemba 13 2010 kuugua kwa muda mrefu na alifariki Dunia.
Remmy ambaye jina lake kamili ni Ramadhani Mtoro Ongala alikuwa ni kati ya waimbaji walioweza kuandaa tungo zilizosisimua Zaidi mbali na kuwa alikuwa na upekee wa uwasilishaji kama mwimbaji.
Remmy Ongala alifanya vizuri na nyimbo zake nyingi ambazo miongoni mwake ni pamoja na ‘Kipenda Roho’, ‘Karola’, ‘Kifo, Sauti Ya Mnyonge’, ‘Mariam Wangu’, ‘Usingizi’, ‘Pamella’ na nyinginezo nyingi zilizofanya vizuri Zaidi.
Moja ya wazo lake lililosisimua pia nia pale alipoanzisha mashindano ya watu wenye sura mbaya na mbali na kuwa aliamini kuwa yeye ni mwenye sura mbaya zaidi, bado hakuibuka mshindi kwenye mashindano hayo.
Remmy aliposhiriki mashindano alipigwa chini na mtu mwenye sura mbaya zaidi yake na ushindi ulenda kwa mtu mmoja aliyejulikana kama Masoud Sura Mbaya.
Hakika pengo aliloacha Remmy Ongala haliwezi kuzibika.