Aliyekuwa Kocha Mkuu wa zamani wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameibuka na kumchana Mbelgiji huyo kuwa sio kocha.
Eymael ameachishwa kazi kutokana na vitendo vyake vya kibaguzi pamoja na matamshi yasiyo ya kiuungwana ambayo aliyasambaza jana, Julai 26 baada ya kumaliza kusimamia mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli na kushinda bao 1-0.
Zahera amesema kuwa kwa mwenendo wa Eymael ulivyokuwa hakuwa na maisha marefu ndani ya kikosi cha Yanga hata nje hawezi kudumu akipata timu.
"Aina ya makocha kama yule wa Yanga ambaye amefukuzwa ni miongoni mwa makocha ambao hawawezi kufanya kazi Ulaya kwani hakuwa na maneno mazuri kwa waandishi pamoja na vitendo vyake.
"Kwa kuwa amefukuzwa basi ni wazi kuwa akipata timu sehemu nyingine hawezi kudumu, ili uwe kocha mzuri ni lazima uwe na nidhamu katika kile unachoongea," amesema.