Nape asimulia jinsi Mkapa alivyomuokoa asifukuzwe chuo na CCM


Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, amesema Rais Benjamin Mkapa alimuokoa asifukuzwe shule kwa kukosa ada na asiondolewe kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM).

Nnauye aliandika ujumbe huo jana katika ukurasa wake wa twitter kuwa “Nimefanikiwa kumsindikiza kupumzika mtu aliyeokoa nisifukuzwe shule kwa kukosa ada na aliyeokoa nisifukuzwe/nisiondoke CCM! pumzika mzee Mkapa, Msalimie Mzee Nnauye mwambie umemaliza kazi aliyokuachia kwangu! asanye sana,”.

Nnauye ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM amesema mwaka 2001/2002 akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Jamii Kivukoni kwa sasa ni Mwalimu Nyerere, Mzee Moses Nnauye  alifariki dunia Desemba 6, 2001.

“Wakati anafariki sikuwa nimelipa ada ya chuo kwa mwaka husika nilitakiwa kulipa ada ama kuondoka choni kwasababu sikuwa nimelipa ada. Wakati najiandaa kuondoka Mwenyekiti wa bodi ya chuo alikuwa mzee Rashid Mfaume Kawawa  na Makamu wake alikuwa mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mzee Kawawa alipoambiwa alimwelekeza mzee Ngombale kushughulikia na ndipo swala hili lilipofika kwa Mzee Mkapa” aliandika Nape.

Aliongezea kuwa “Kupitia kwa mshauri wake wa mambo ya siasa mzee Ngombale. Mzee Mkapa aliniita na baada ya mazungumzo aliniambia usiache masomo, utalipiwa masomo yako mpaka umalize chuo. kuanzia hapo nikaanza kulipiwa masomo yangu Kivukoni mpaka nikamaliza huyu ndio mzee Mkapa aliyelala leo,”

Nape alisema suala la CCM atalielezea leo panapo majaliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad