NYOTA ya Rais John Magufuli inazidi kungaa baada ya Mtabiri wa mambo ya nyota jijini Dar es salaam Sharif Bawazir kumtabiria ushindi wa kishindo katika chaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika nchini kote Oktoba Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mnajimu huyo mbali na kutabiri ushindi huo kwa Rais Magufuli, pia alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika hali ya utulivu na amani ikilinganishwa na miaka mingine yote ambao uchaguzi huo umewahi kufanyika.
“Ni uchaguzi unaoonekana kutokuwa na upinzani mkubwa kwa Rais Magufuli kutokana na nyota yake kuwa juu, kutokana na mambo ya kinyota kuonyesha kuwa hatopata upinzani wenye nguvu kutokana na kuonekana kupendwa na watu wengi ikichangiwa na utu wake kwa watu wanyonge” alisema Bawazir
Hata hivyo Mnajimu huyo ametabiri anguko kubwa la wabunge waliokuwemo katika Bunge lililopita na kudai kuwa sura mpya ndizo zitakazotawala katika bunge hilo kutokana na muonekano wa kinyota kwa kipindi hiki kuonyesha kuwa waliokuwemo bungeni msimu uliopita wengi wao nyota zao zimeshuka.
Alisema hiyo ni kutokana na sababu za kimahesabu yanayowahusu wagombea hao wa kuonyesha kuwa hawatoweza kutetea nafasi zao tofauti na ilivyokuwa kwa mgombea wa nafasi wa urais anayeonekana kukubalika ambapo ili kuweza kurudi tena amewashauri kufanya maombi makubwa ya kidua ili kuondoa mikosi waliyonayo.
“Kuna sababu ya wao kufanya dua ili kuwawezesha kuondokana na mikosi katika nyota zao, tofauti na hivyo bunge lijalo linakwenda kushuhudiwa sura mpya zikitawala, haya yanawezekana kwa kuwa yote ni masuala ya kinyota” aliongeza Mnajimu huyo
Pamoja na mambo hayo Bawaziri pia aligusia namna mbavyo Tanzania ilivyofanyikwa kupamba na ugonjwa hatari wa virusi vya Corona kwa kusema kuwa mafanikio hayo yamekuja baada ya taifa zima kujielekeza kwa Mungu kimaombi.
Alisema kutokana na hatua hiyo iliyochagizwa na msimamo wa Rais Magufuli, kulilifanya taifa zima kwa ujumla wake kumuomba Mungu na hivyo kumfanya asikie kilio hicho ., suala lililofanikiwa na kuuondoa ugonjwa huo kwa watanzania.