Katibu Mkuu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey polepole amesema waliofungana katika kura za maoni wasiwe na hofu wao wataendelea na mchakato wao wa vikao kuweka mapendekezo.
Polepole ametoa kauli hiyo baada ya watia nia kufungana matokeo katika kura za uchaguzi za wagombea katika majimbo.
“Limekuwepo swali katika kura hizi za maoni kuwa kuna maeneo mengine ambapo wagombea wamefungana kwa idadi ya kura mfano Mwibara , Sengerema sasa hiii isiwaletee hofu,”amesema Polepole.
Aliongozee “Sisi hatutafuti mshindi katika kura za maoni tunataka kutoa nafasi kwa wanaCCM kutoa maoni yao ya awali ambayo yatasaidia vikao vya mbele kuweka mapendekezo yao na hatimaye kufanya uamuzi,”
Polepole amesema hata kama wamefungana uchaguzi hauwezi kurudiwa wataendelea na vikao vya kuweka mapendekeza.