Profesa Jay Hataki Mchezo Kabisa Kwenye Suala la Ubunge Atuma Ujumbe Nzito CCM

Mbunge wa jimbo la Mikumi anayemaliza muda wake Joseph Haule (Profesa Jay) ametuma ujumbe kwa makada wa chama cha mapinduzi waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kwenda kugombea ubunge kwenye jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka mitano.

Haule ametuma ujumbe huko kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuanza kwa mchakato wa ndani kuchaguliwa kwa wagombea hao ikiwa ni hatua ya awali ya kuchagua wagombea watakao shindana na Haule kwenye uchaguzi ujao.

“Mikumi Stand uo, Nasikia hapa Mikumi wapo 50 namsubiri sana huyo kinara wao Huko kwenu kuna habari gani “ ameandika Joseph Haule.

Ikumbukwe zoezi la kupitisha wagombea kwenye ngazi ya awali ya jimbo imeanza rasmi leo Julai 20,2020 ikiwa ni sehemu za mwanzo za kuchagua wagombe watakao peperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad