Rais Uhuru Kenyatta apiga marufuku uuzaji wa pombe Kenya kwa siku 30


Hakutakuwa na uuzaji wa pombe katika mikahawa na maeneo ya kuuza vyakula kwa kipindi cha siku 30 zijazo, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. 


Rais Kenyatta amesema kwamba baa zote zitafungwa mara moja akiongezea kwamba zile ambazo zitakiuka agizo hilo jipya zitapokonywa leseni zao. 


"Baa zitakazokiuka agizo hilo zitapokonywa leseni zao'' , alisema Uhuru. 


''Masharti yote ambayo ninayatangaza yataheshimiwa na Wakenya wote bila kujali nyadhfa zao katika jamii'', aliongezea. 


Aidha rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na moja alfajiri itaendelea kuwepo kwa kipindi chengine cha siku 30. 


Amewataka Wakenya kufutilia mbali dhana potofu kwamba viwango vya chini vya vifo vina maana kwamba ugonjwa jhio sio hatari. 


''Tatizo letu ni kuongezeka kwa wagonjwa wanaoambukizwa virui hivi na katika maeneo kwa mfano kama nairobi ugonjwa huu umeongezeka sana ,vijana wamekuwa wakiwaambukiza wazazi wao'' ,alisema. 


Amesema kwamba vitendo vya hatari vinavyotekelezwa na vijana wakati huu vimehatarisha maisha ya wengine katika jamii. 


Ongezeko la wagonjwa wa covid-19 linajiri baada ya hotuba yake ya tarehe 6 mwezi Julai ambapo aliondoa baadhi ya masharti ikiwemo kuruhusu watu kutoka katika kaunti zilizotajwa kuwa na maambukizi ya juu kama vile Nairobi, Mandera na Mombasa kusafiri. 


Tatizo limekuwepo katika udhabiti wa kiuchumi huku mashirika mengi yakiwafuta kazi watu wengin na wengine wakipunguza mishahara ya wafanyakazi wao mbali na wafanyabiashara kukadiria hasara kubwa kutokana na marufuku ya mikusanyiko ya watu. 


Kaunti 44 kati ya 47 tayari zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona . 


Ni kaunti ya Baringo , ile ya Pokot magharibi na ile ya Mandera ambazo hazijawahi kuripoti mgonjwa wa corona. 


Mwezi uliopita , rais Uhuru Kenyatta aliondoa usafiri wa Nairobi, Mombasa na Mandera kutoka Juni 7 2020. 


Hatahivyo rais Kenyatta aliongeza masharti ya kutotoka nje kati ya mwendo wa saa tatu usiku hadi saa kumi na moja alfajiri kwa siku nyengine 30 zaidi. 


Uhuru ambaye alitoa agizo hilo la kuondolewa kwa baadhi ya masharti hayo alionya kwamba iwapo hali itazorota na kutoa changamnoto kwa sekta ya afya , atarudisha masharti hayo. 


Wakati huohuo wizara ya afya nchini Kenya imetangaza kwamba wagonjwa wengine 440 zaidi wameambukizwa virusi vya corona na kufanya idadi ya walioambukizwa nchini humo kufikia 17,975. 


Katika taarifa yake, waziri wa Afya Mutahi Kagwe aliripoti kupimwa kwa sampuli 3,197 katika kipiundi cha saa 24, na kuongeza jumla ya idadi ya sampuli zilizopimwa nchini kufikia 279.612. 


Mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi alikuwa mtoto wa miaka mmoja huku mzee kabisa akiwa na umri wa miaka 84. Wagonjwa wanawake waliripotiwa kuwa 154 nao wale wa kiume wakiwa 286. 


Raia wa Kenya walioripotiwa ni 437 huku waliosalia wakiwa raia wa kigeni. Waziri Kagwe vilevile alitangaza watu watano zaidi waliofariki kutokana na ugonjwa huo hatua inayoongeza idadi hiyo kufikia 285 huku watu wengine 90 wakiripotiwa kupona na kuweka idadi ya waliopona kufikia 7,833.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad