Rais wa Malawi Akosolewa kwa Kuteua Ndugu zake Kwenye Baraza la Mawaziri



Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri lialojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu

Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi

Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo

Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake

Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera ana wafuasi wengi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad