Zaidi ya wanachama mia tano wa Chama cha Mapinduzi wamejitokeza mkoani Morogoro, kutia Nia ya kuwania nafasi ya Ubunge katika majimbo 11 ya mji huo.
Akitoa takwimu hizo Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa waliojitokeza kutia nia majimbo 11 Mkoa wa Morogoro ni 457 wanaume 393 na 64 wanawake, Morogoro Mjini 82, Morogoro Kusini 23, Morogoro Kusini Mashariki 22, Mvomero 60, Gairo 21, Kilosa 29 , Mikumi 47, Kilombero 62, Mlimba 39, Malinyi 34 na Ulanga 38.
Shaka ameongeza kuwa, "Viti Maalum Wanawake (UWT) 105, Vijana 15 , Wazazi 15 maandalizi kwa ajili ya kura za maoni tarehe 20- 21 Julai 2020, yanakwenda vizuri na wajumbe wote wa mikutano mikuu wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ambapo CCM Mkoa wa Morogoro tumejipanga vyema ili kuhakikisha zoezi linatawali na haki, uhuru na amani ili kutimiza dhana ya demokrasia pana na iliyotukuka ndani ya Chama chetu”.
Julai 16, 2020 Akiwaapisha viongozi aliowateua Ikulu ya Chamwino, Dodoma Rais Magufuli alisema kuwa mpaka siku ile zaidi ya watia Nia elfu nane wa Ubunge walikuwa wameshachukua fomu nchi nzima kupitia chama cha mapinduzi.