MATOKEO ya kura za maoni kwa wagombea nafasi za Ubunge na Uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambayo yameanza kutangazwa leo yameonyesha baadhi wa vigogo wa kisiasa visiwani unguja wameangushwa akiwemo Saada Mkuya Salum akigombea jimbo la Kikwajuni.
Mbali na Saada Mkuya aliyeshindwa na Nassor Salim Ali katika nafasi ya Uwakilishi ambaye alipata kura 34 huku yeye akipata kura tisa mwingine aliyeangushwa katika kura hizo za maoni ni Mattar Ali Salum ambae alikuwa Mbunge wa Jimbo la Shauri Moyo Unguja.