Sayari mbili kubwa' zaidi zenye uhai zagunduliwa karibu na mfumo wa jua




Sayari mbili zaidi zimegunduliwa na kundi moja la wanasayansi wa kimataifa karibu na mfumo wa jua. 

Na kuna uwezekano wa sayari nyengine ya tatu karibu na sayari hizo mbili. 

Sayari zote mbili zinazunguka kwa ukaribu -nje ya eneo lenye uhai kwa jina GJ887 - nyota ndogo iliopo umbali wa miaka 11 ya mwanga wa jua. 

Ukaribu uliopo kati ya sayari hizo mbili na nyota - ni mkubwa kuliko ukaribu kati ya Mercury na jua. 

Sayari hizo mbili ambazo uwepo wake umethibitishwa , zimetajwa kuwa 'dunia kubwa' . 

Zina ukubwa ambao ni mara 4 na saba zaidi ya dunia, lakini ziko sawa na Uranus na Neptune. 

''Pia zimedaiwa kuwa na msingi dhabiti'' , amesema Sandra Jeffers wa chuo kikuu cha Gottingen na kiongozi wa utafiti huo, akizungumza BBC. 

Sayari hizo zinaaminika kuwa na mazingira yenye uzito ikiliganishwa na dunia yetu. 

Utafiti huo ulifanywa na mradi wa Red Dots, na kubuniwa na vyuo mbalimbali duniani ili kutafuta sayari zinazofanana na dunia na zilizo karibu na mfumo wa jua na matokeo yake yakachapishwa katika jarida la sayansi . 

Je ni nini kinachojulikana kuhusu dunia hizi mbili zilizopo karibu? 

Sayari zote mbili, zilizopewa majina ya GJ 887b na GJ 887c, ziligunduliwa kwa kutumia chombo chenye mionzi ya kiwango cha juu kinachotafuta sayari European Southern Observatory (ESO) kilichopo huko La Silla, nchini Chile. 

Kulingana na uchunguzi, sayari hizo mbili zipo karibu na nyota yao. 

Ile iliopo mbali na nyota hiyo, GJ 887c, huchukua takriban siku 21.8 za dunia ya kawaida kufanya mzunguko mmoja na GJ 887b huchukua siku tisa 9.3 za duniani kukamilisha mzunguko mmoja katika jua. 

Mizunguko hiyo ni ya kasi na mifupi ukilinganisha na sayari ya Mercury ambayo huchukua siku 88 za duniani kukamilisha mzunguko mmoja katika jua. 

Wataalam wa angani tayari wamegundua sayari nyengine zilizopo karibu na mfumo wa jua kama vile Proxima Centauri na Wolf 359, iliopo umbali wa miaka 4.2 na 7.9 ya mwanga mtawalia. Lakini hazipo karibu sana kama vile GJ887. 

Hivyobasi sayari ya GJ887 ndio ilio karibu zaidi. Lakini GJ887 ndio iliojikusanya karibu zaidi , kulingana na taasisi ya fizikia ya angani Andalusia (IAA-CSIC. ilioshiriki katika utafiti huo.. 

''Mifumo hii ya sayari hupatikana sana katika nyota nyingine - kati ya asilimia 15 hadi 30 ya nyota ya solar-type - lakini hatujawahi kuona moja ilio karibu sana na jua," alisema Guillem Anglada-Escudé, kutoka taasisi ya sayansi ya angani (ICE-CSIC) kutoka chuo kikuu cha Barcelona na mmoja wa wwanzilishi wa utafitoi huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad