Serikali kutumia Mil 400 kujenga shule mpya ya kumuenzi Mkapa

 

Wakati shughuli ya kuuaga Mwili wa wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamini  Mkapa ukiendelea uwanaja wa Uhuru Jijini Dar e salaam,Serikali ya awamu ya tano imetenga kiasi cha Fedha cha Shilingi Milioni 400 kujenga shule mpya na ya kisasa kijijini Lupaso. 


Hayo yamethibitishwa na aliyekuwa Diwani wa kata ya Lupaso Dogras Mkapa amabye ni mtoto wa Mdogo wa Mraehemu ambapo amesema kuwa fedhi hizo tayari zimishatolewa na Serikali na mara baada ya taratibu za mazishi kukamilika na mchakato wa ujenzi wa shule hiyo utaanza Rasmi. 


Aidha Dogras Mkapa amechukua fursa hiyo kwa kumpongeza Rais John Pombe magufuli na Serikali yake ya awamu ya Tano  juu ya kutenga kiasi hicho cha Fedha ili kuijenga shule hiyo na iwe kumbukumbu kwa Hayati Benjamini Mkapa. 


Lakini pia Dogras ameongeza kuwa wao kama familia wamepokea kwa masikitiko juu ya kifo cha Rais Benjemini Mkapa kwani kuna miradi mingi aliyotaka kuitekeleza kijijini hapo ikiwa ni pamoja na  ujenzi wa Zahanati, maji Nk. 


Huku sifa kubwa aliyokunayo Mzee mkapa ni pamoja mcha mungu ,mpenda Amani na manengeleo hivyo Dogras amewasihii watanzania kuendelea kuyaenzi mema yote aliyekuwa anayafanya enzi za utawala na uhai wake. 


“Niishukuru Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe Rais wetu Magufuli kwa  kazi mzuri anazozifanya kwa ajili ya watetezi kwa wanyonge hivi sasa ninavyozungumza hapa tumeweza kupata fedha Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule Mpya ya kisasa  kwa ajili ya kumuenzi Rais wetu Benjamini Mkapa”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad