Sheria ya kumiliki laini moja kwa kila mtandao yaanza




Sheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni kuzuia kumiliki laini ya simu zaidi ya moja kwa mtandao mmoja wa simu imeanza kutumika jana, Julai 1, 2020. 

Kwa mujibu wa sheria hii, ikibainika unamiliki laini zaidi ya moja kutoka kampuni moja ya simu, adhabu yake ni faini ya Tsh. Milioni 5 au kifungo jela mwaka mmoja au vyote kwa pamoja na katika kila siku ambayo laini ya ziada ilitumika mhusika atalipa faini ya Tsh. 75,000 kwa siku. 

Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada. Lengo ni kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na kudhibiti uhalifu. 

Aidha, sheria hairuhusu kampuni kumiliki laini zaidi ya 30 ambazo zitatumika kupiga, kutuma jumbe au huduma ya intaneti. Endapo kampuni itakiuka itatozwa faini isiyopungua Tsh. Millioni 50 pamoja na Tsh. 175,000 kwa kila siku ambayo laini za/ya ziada ilitumika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad