Shigongo, Tizeba Wafungana Kura za Maoni Buchosa


WATIA nia wawili katika Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric James Shigongo na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Charles Tizeba wamefungana idadi ya kura za maoni ambapo kila mmoja amepata kura 354.


Zoezi la kupiga kura limefanyika leo Jumatatu, Julai 20, 2020 katika eneo la Nyehunge lililopo Halmashauri ya Buchosa huku kukishuhudiwa jumla ya wajumbe 755 wakipiga kura kwa wagombea 34, hivyo wagombea hawa wawili wameongoza kwa kuwa na jumla ya kura zinazolingana idadi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad