Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la #CoronaVirus ni dharura mbaya zaidi ya kiafya kutokea duniani
Amesema dunia inaweza kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ikiwa taratibu mbalimbali za kiafya ikiwemo kuvaa barakoa zitazingatiwa huku akizipongeza nchi za Canada, China, Ujerumani na Korea Kusini kwa kudhibiti mlipuko
Hadi kufikia leo, jumla ya mambukizi 16,397,921 na vifo 651, 675 vimerekodiwa huku idadi ya wagonjwa waliopona ikifikia 9,810,294. Mataifa yaliyoathirika zaidi ni Marekani, Brazil, India, Urusi na Afrika Kusini