Shirika la UN lasema meli ''iliyotekwa'' inayotafutwa na Marekani sasa iko Iran


Shirika la Kazi DUniani, (ILO) limesema leo kuwa meli ya mafuta iliyokuwa ikitafutwa na Marekani iliyokuwa ''imetekwa'' katika Pwani ya Umoja wa Falme za Kiarabu baada ya madai ya kuingiza kinyume cha sheria mafuta ambayo hayajasafishwa kutoka Iran, imerejea katika pwani ya Iran. 


Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kuwa meli hiyo aina ya MT Gulf Sky ilitekwa nyara mnamo Julai 5 ikimnukuu nahodha wake. Matamshi hayo yanalingana na ripoti za awali za shirika la habari la Associated Press. 


Shirika la ILO limeongezea kuwa meli hiyo ilipelekwa Iran na kwamba wafanyakazi wake 28 kutoka India walishukia nchini humo huku wafanyakazi wote isipokuwa wawili waliokosa pasipoti wakisafiri kwa njia ya ndege kutoka Iran kuelekea India mnamo Julai 15. 


Shirika la habari la serikali ya Iran na maafisa wa serikali hiyo hawajathibitisha kutekwa nyara na kuwasili kwa meli hiyo nchini Iran. Serikali ya Marekani pia haijatoa tamko lolote.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad