Simu imetowesha amani katika familia yangu. Naitegemea 90% katika kazi zangu za kila siku



Zaidi ya asilimia 90 ya shughuli zangu za siku zinategemea matumizi ya simu. Lakini simu hii imekuwa inaniletea ugomvi wa mara mwa mara nyumbani, kila siku ugomvi.

Shida ni kwamba mke wangu amekuwa akichukua simu yangu mara kwa mara na kuanza kuikagua, akiona namba yenye mashaka basi ataanza kuhoji na kumpigia muhusika. Mara nyingine nimekuwa mbabe na hata kumpiga na kumwambia aachane na simu yangu lakini anarudia tabia hiyo hiyo.

Ukiweka password nayo ni maneno na malumbano kwamba kuna mambo naficha. Ni kweli nachepuka ila sio kwa kiwango hicho anachonidhania.

Nimetafuta alternative ya kuweza kuwasiliana na wadau wangu wa kazi na watumishi wenzangu bila simu nimeshindwa lengo likiwa ni kuachana na matumizi ya simu kabisa.

Je mwanamke huyu nimfanyaje? Kwanini hakomi kunifuatilia kwa undani katika mawasiliano yangu?
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tena shukuru una mke anayekupenda kwa dhati ndiyo maana anakufuatilia ili usije kumletea magonjwa ndani ya ndoa, cha muhimu acha kuchepuka na kuwa mwaminifu kwenye ndoa,mke ana haki ya kujua kila unachokifanya sasa ukisema asiguse simu yako maanavyake wewe si mwaminifu ndani ya ndoa yako, kuwa makini sana unachokifanya kinahatarisha uhai wa ndoa yako, kumpiga huyo mwanamke wala hakusaidii bali kutaongea matatizo zaidi.

    ReplyDelete
  2. Ninachokushauri usitumie ubabe, wewe jifanye mjinga kuwa mpole ikiwezekana mnunulie kitu kizuri mpe, mbusu, mkumbatie tuliza huo mgogoro, zidisha upendo kwake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad