Mwanamke huyo anaweza kuondoka kwenda mizunguko yake kisha anamuacha mtoto nyumbani huku mbwa huyo mpole, mtiifu, na mnyenyekevu akimlinda mtoto na kucheza nae na mwanamke huyo anaporudi anakuta mtoto kalala usingizi mzito pamoja na mbwa huyo.
NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA
Siku moja mwanamke alienda sokoni na kama kawaida yake akamuacha mtoto pamoja na mbwa.
Aliporudi, aligundua kuna jambo la kutisha sana, vitu vilikuwa vimevurugika ndani hatari, mbaya zaidi mtoto hakuwa kwenye kitanda chake cha kubembea. Damu zilikuwa zimetapakaa kwenye kitanda cha mtoto na kwenye kabati yaani kwa ufupi chumba kizima kilikuwa na damu.
Mwanamke huyo alianza kumtafuta mtoto chumbani humo kila kona, Ghafla mbwa huyo akajitokeza kutoka chini ya kitanda akijilamba ulimi na akitikisa mkia na kichwa kama umbwa alietoka kula msosi wa hatari.
Moja kwa moja mama huyo akafikiria kuwa mbwa atakuwa kamaliza kumla mtoto wake, akachukua ukuni mkubwa akampiga kipigo cha adabu mbwa huyo mpaka akamuua.
Kisha aliendelea kumtafuta mtoto wake huku akiwaza kuwa hata akipata kiungo kimoja cha mtoto wake itakuwa afadhari tu.
Ghafla tena chini ya kitanda humohumo akamuona mtoto wake akiwa salama kabisa bila kovu lolote huku akiwa na tabasamu,
NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA
Kwa hofu kubwa tena akaona nyoka mkubwaaa akiwa anavuja damu huku kichwa chake kikiwa kimetengana na mwili. Ilikuwa ni vita kubwa kati ya nyoka na mbwa, na yote haya mbwa alifanya ili kuhakikisha usalama wa mtoto.
Lakini tayari kutokana na kutokuwa mvumilivu pamoja na kuwa na hasira za haraka akawa amemuua mbwa mwaminifu, mpole, mnyeyekevu.
--------------
Ni mara ngapi tunawahukumu watu kwa maneno mabaya na kuwatendea vitendo vya uovu bila kuchukua mda na kufanya tathimini????
Kwako wewe unaesoma post hii, Naomba Mungu akusamehe kwa neema yake kutokana na makosa ambayo unafanya bila kufikiria lakini bado anakupenda na unazidi kupata neema ya uhai.