Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na Kuwatumia Nyoka Badala ya Kuwaua..!!!



Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.

Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1.zingatia hali ya joto na hewa .

Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,

2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara

Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.

3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.


Faida 3 za ufugaji wa nyoka

1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.

2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.

Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka.

Mwisho sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao!! Waangamizwe hadi waishe. Tutauza maparachichi is a pamba, korosho, embe, machungwa, nazi nk

    ReplyDelete
  2. Nyoka ni kiumbe kisichokuwa na tatizo na binadamu,nyoka ameharibiwa sifa na hivi vitabu vya kifedhuli yaani KORAN NA BIBLIA,




    ReplyDelete
    Replies
    1. Last week tumesoma mtu amekufa kwa kuumwa na nyoka huko namtumbo

      Delete
  3. Hujaongelea Namna ya kujilinda kutokana na hatari zao kwakuwa nyoka husababisha vifo vingi

    ReplyDelete
  4. Katika ya mambo niliyokuwa nayangoja ni hili. Nahitaji kifuga nyoka nifanyeje?

    ReplyDelete
  5. Katika ya mambo niliyokuwa nayangoja ni hili. Nahitaji kifuga nyoka nifanyeje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi pia vip unefikia hatua gani had sas

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad