Mchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa Bernard Morrison hapaswi kuwa mkubwa kuliko timu hivyo lazima uongozi uweke usawa katika hili.
Mayay amesema kuwa kutokana na mvutano uliopo kwa sasa kati ya Yanga na mchezaji huyo Morrison ilipaswa mambo yamalizwe kitaalamu na kila kitu kiwekwe sawa kabla ya kumrejesha kwenye kikosi.
Mchambuzi huyo ameongeza kuwa hakuna mafanikio ambayo mchezaji anaweza kuyapata ikiwa hatakuwa na timu hivyo ni lazima aiheshimu timu.
"Ni lazima mchezaji asiwe juu ya klabu kwa namna yoyote ile inaharibu na kupoteza uhalisia wa maisha ya wachezaji na ndio jambo ambalo huwa linawaumiza wachezaji wengine.
"Kwa suala la Morrison ilipaswa uongozi wa Yanga uweke mambo yanayoendelea bayana ili mashabiki wajue kuna nini ambacho kinaendelea.
"Ukitazama hakuna mchezaji ambaye amewahi kujulikana ikiwa hana timu hivyo ili aweze kupata mafanikio ni lazima awe na timu ambayo ni kubwa kuliko mchezaji," amesema Mayay.
Morrison jana alirejea kikosini na kuanza mazoezi na wachezaji wenzanke ambao leo wameanza safari kuelekea kwenye mchezo wa Biashara United.