Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA),alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya Umeme cha AfriCAB alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akiangalia bidhaa kutoka kwa wajasiriamali wanaofadhiliwa na Benki ya Biashara Tanzania (NBC), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Bidhaa zinazotokana na zao la Mkonge ambazo zinauzwa katika banda la Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) lililoko katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa Habari alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Dkt.Ng’wanza Kamata (Mwenye miwani) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bi.Latifa Khamis (wa pili kulia) alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
*******************************
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO
Serikali imewataka Wananchi kuendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwani chanzo cha nchi kufikia uchumi wa kati ni pamoja na wananchi wake kupendelea bidhaa ambazo wanazizalisha wao kama wao, na mafanikio yametokana na juhudi za watanzania wote wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayofanyika katika Uiwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa ili watanzania waweza kusheherekea mafanikio endelevu ya kuingia nchi zenye kipato cha kati wanatakiwa kuwa wa kwanza kutangaza bidhaa zao.
“Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya ya nchi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye kipato cha kati yawe ni matunda kwa watanzania hasa kwa wakina mama na vijana wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania”. Alisema Mhe.Bashungwa.
alisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuangalia bidhaa za ndani Kabla hawajanunua bidhaa kutoka nje ili kuweza kukuza viwanda na kuwa na uchumi wenye kipato cha kati endelevu kwani ili Watanzania waendelea kusheherekea mafanikio haya ya kufikia kipato cha kati tunatakiwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Alibainisha kuwa kupitia maonesho 44 ya Biashara kimataifa (sabasaba) ambapo takribani kampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi zitashiriki, kutakuwa na fursa ya wananchi kuja kununua bidhaa na kuangalia teknolojia mbalimbali zikioneshwa na taasisi na makampuni ya kitanzania, pia kupitia B2B wale ambao wapo nje wataendelea kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wanashiriki katika maonesho ya sabasaba hayo.
Pamoja na hayo Mhe. Bashungwa amesema Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati inasaidia kuingia kwenye rada ya kimataifa hivyo wengi watapenda kuja kuwekeza hapa nchini