Serikali ya Kenya jana imetangaza kupunguza ada za kuingia Mbuga Kuu za Wanyamapori kwa Watalii kutoka ndani na nje ya nchi ili kufufua sekta ya utalii iliyoathiriwa sana na janga la COVID19
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Huduma za Wanyama Pori nchini Kenya (KWS) limesema hatua hiyo itadumu kwa mwaka mmoja
Pia, shirika hilo limewaruhusu wamiliki wa nyumba za kulala wageni kwenye Hifadhi za Wanyamapori wasitishe kulipa kodi kwa mwaka 1 kuanzia tarehe Mosi mwezi Julai hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka ujao
Waziri wa utalii, Najib Balala amewataka wamiliki hao kuboresha huduma za watalii na kukuza biashara zao kwa kutumia akiba inayotokana na usitishaji wa kodi