Tatizo la Kutokwa na Majimaji Kwenye Matiti


Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba. Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale  yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.

Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.

Chanzo cha tatizo
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.

Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone.

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.

Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu  na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.

Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.

Uchunguzi
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.

Ushauri
Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad