Uchaguzi 2020: Ushauri kwa CHADEMA kuelekea Oktoba 2020



Andaeni ajenda msiandae wagombea. Wagombea wakipatikana kupitia michakato mliojiwekea watembee katika ajenda zenu kuu kulingana na jinsi nchi ilivyo kwa sasa. Msifanye wagombea kua ajenda hamta pata kura.

Hamuwezi kupata kura nyingi katika mazingira ya huruma "public sympathy" kama ambavyo sasa inaonekana bila ajenda zitakazotokana na mapungufu ya selikali ya sasa.

Ile dhana inayozidi kujengeka kwamba kura zitapatikana kwa kuwa "Mgombea" alipigwa risasi na alifanyiwa hila italeta siasa lakini haitaleta kura kwa kizazi cha sasa ambacho "unemployment rate" ni kubwa mno.
Andaeni na kuanza kuziuza ajenda zenu mbadala za nchi. Ajenda hizo ndizo zitazaa Ilani "manifesto".

Mtakumbuka aenda ya ufisadi ndiyo iliwapa umaarufu. Ufisadi na rushwa kubwa kubwa bado zipo,sijajua kwanini mliachana na hii ajenda. Jitahidi kuelekea kampeni kuja na programu ya kupata mawazo ya wananchi kupitia platforms mbalimbali nchi nzima ili mpate ajenda itakayo zaa ilani nzuri yenye kugusa makundi yote na iitwe ilani ya wananchi sio ya chama ili mgombea wenu aje aiuze kwa wananchi.

Chama chenye wanachama,madiwani na wabunge nchi nzima kinaweza kuandaa programu ya kupata mawazo ya wananchi,mawazo yakachambuliwa ikapatikana ilani nzuri yenye ajenda za kugusa maisha ya wananchi.

Hii ni kwa vyama vyote: vyama viondokane na ile "dhana" ya watu flani "wasomi" kuweka mawazo yao katika karatasi na kuyaita "ilani" au "manifesto" na kuja kuiuza kwa wananchi.

Ilani angalau itokane na mawazo ya wananchi hata kwa asilimia 80% ndipo mtapata uungwaji mkono. Fikiria ishu ya ukosefu wa ajira kwa sasa ni ishu kubwa sana kuliko inavyofikiriwa au kuchukuliwa na watawala.

Kuwaacha wagombea kuwa ajenda kutaleta siasa lakini hakuwezi kuleta kura na uungwaji mkono mkubwa. Itikadi,falsafa,ajenda na sera ndio moyo wa siasa za chama chochote.

Nawasilisha.

Aloycious/JF

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad