Uchokozi wa Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran ni ugaidi


Balozi wa Syria mjini Tehran amesema, uchokozi wa ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria ni nembo na dhihirisho la ugaidi wa Marekani dhidi ya raia wakiwemo wanawake na watoto.

Adnan Mahmoud, Balozi wa Syria nchini Iran ametoa taarifa Jumamosi ambapo ametangaza kufungamana na wasafiri wa ndege ya abiria ya Iran na kusema: "Uchokozi wa  ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran katika ardhi ya Syria ni katika hatua za Washington za kuunga mkono magaidi na kupora utajiri wa watu wa Syria."

Balozi Mahmoud ameongeza kuwa: "Kitendo hicho cha Marekani ni ukiukwaji wa wazi wa sheria na kanuni za kimataifa kuhusu safari za ndege zisizo za kijeshi."

Hali kadhalika balozi wa Syria nchini Iran amesisitiza kuhusu udharura wa wanajeshi vamizi wa Marekani na wanajeshi wote ajinabi ambao wako kinyume cha sheria nchini Syria waondoke katika nchi hiyo mara moja kwani uwepo wao ni tishio kwa usalama na uthabiti katika eneo.


Usiku wa kuamkia Ijumaa, ndege mbili za kivita za Marekani zilitatiza safari ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa katika anga ya Syria. Baada ya hatua hiyo hatari na ya kihasama ya ndege hizo mbili za kivita, rubani wa ndege ya abiria ya Shrika la Ndege la Mahan la Iran alipunguza kasi ya mwendo wa chombo hicho, suala ambalo lilisababisha majeruhi kwa baadhi ya abiria. 

Msemaji wa kikosi cha jeshi la kigaidi la Marekani katika eneo la magharibi mwa Asia (CENTCOM), Bill Urban, amekiri kwamba ndege za kivita za Marekani ziliifuata ndege hiyo ya abiria ya Iran lakini amedai kuwa, ni kitendo cha kiufundi kilichofanyika kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad