Nilimuona kama ni mtu mwenye kipaji halisi na sio cha kulazimisha. Niliona ni mtu mwenye sauti ya kufanya mziki wowote iwe Rap au hata kuimba. Nikajiuliza mbona hafahamiki? Mbona media hazioni hiki kipaji badala yake wasanii wa hovyo tu wanapewa airtime.
Nimekuja kumfuatilia mwaka huu nikagundua ujio wake umeshamiri sana. Nimekuta ameanza kuwa maarufu kwenye sanaa ya mziki na ucheshi. Kwa sasa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanyiwa interview na media nyingi sana.Ni moja kati ya watu ambao clips zao hazikosi kwenye mitandao.
Hongera sana Baba Levo.
Hoja yangu sio kusifia Baba Levo bali amekuwa kielelezo cha watu kutokukata tamaa mapema. Katika kutafuta mafanikio ni vyema tukapambana mpaka tone la mwisho. Mafanikio hayaji ghafla tu kama upepo. Kuna milima na mabonde. Hata ukiyapata bado utaihitaji subira kwenda zaidi na zaidi.
VIDEO: