Godbless Lema azungumza na waandishi kuhusu Mo DewjiAliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini (CHADEMA) Goodbless Lema amehaidi kuwa mmoja kati ya wanachama wa CHADEMA watakaojitokeza siku ya jumatatu Julai 27, 2020 kumpokea makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu atakapo wasili nchini.
Lema ameweka wazi uamuzi huo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wa twitter ambako amesema kitendo cha Lissu kurudi nchini ni mapenzi na miujiza ya Mungu.
“Nilimuuliza haugopi?akajibu siogopi!Nikamwambia,wanaweza kukupiga risasi tena au ukafungwa kwa hila,akajibu NIKO TIYARI kwa lolote.Mungu ni mwema,Kamanda Tundu Lissu kurudi nyumbani kwa mapambano tena ni muujiza wa Mungu mwenyewe.Nitakuwepo Dar es Salam kumpokea siku ya jumatatu “ ameandika Lema
Makamu mwenyekiti wa hicho alitangaza kurejea nchini baada ya miaka mitatu ya kukaa nje baada ya kupingwa risasi na watu wasiojulikana akiwa njiani kwenda nyumbani kwake jijini Dodoma.
Nilimuuliza haugopi?akajibu siogopi!Nikamwambia,wanaweza kukupiga risasi tena au ukafungwa kwa hila,akajibu NIKO TIYARI kwa lolote.Mungu ni mwema,Kamanda Tundu Lissu kurudi nyumbani kwa mapambano tena ni muujiza wa Mungu mwenyewe.Nitakuwepo Dar es Salam kumpokea siku ya jumatatu
— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) July 23, 2020