Katika barua jana, Marco Rubio. Tom Cotton na wabunge wengine walielezea madai ya uchujaji taarifa unaofanywa na Tik Tok wa maudhui nyeti, ikiwa ni pamoja na video inayokosoa China inavyowatendea Waislamu wa kabila wa Uighur ambao ni wachache pamoja na madai ya jaribio la Beijing kuvuruga majadiliano ya kisiasa katika app hiyo ya mtandao wa kijamii.
Wabunge hao waliandika katika barua hiyo kuwa wana wasi wasi mkubwa kwamba chama tawala cha Kikomunist cha China kinaweza kutumia udhibiti ilionao wa Tik Tok kuvuruga ama kushawishi mazungumzo ili kusababisha mgawanyiko miongoni mwa Wamarekani na kufanikisha lengo lao kisiasa