Kuna sababu nyingi zimetolewa kwa vijana kushindwa Kuoa na Kuolewa, nyingi kati ya hizo ni za kiuchumi na kujifanya wanajipanga kimaisha.
Ukweli ni kwamba watu wengi hawaingii kwenye Ndoa kwa sababu wanapata kirahisi tendo lenyewe la Ndoa.
Msingi wa Ndoa sio tendo la Ndoa pekee, kunafaida nyingi katika Ndoa hilo liko wazi kabisa.
Lakini ukwel ni kwamba tendo hili la ndoa lina msukumo wa pekee na ushawishi mkubwa katika kuanzisha mahusiano ya ndoa.
Maeneo ambayo vija upenda kupunguzia mahitaji yao ya Ndoa ni kwenye Madanguro, Bar, Massage parlour, makaburini.
Ukweli kungekuwa na Tamaduni au Sheria kali zinazodhibiti matendo ya Ndoa holela ndoa zingekua nyingi.
Ni ukosefu wa elimu bora kwa jamii hasa vijana juu ya manufaa ya ndoa. Ndoa inafaida nyingi tu sio ngono peke yake. Ngono inayozungumziwa hapa ni zinaa au uasharati na ndio chanzo cha ufukara na maradhi kwa mwanadamu.
ReplyDeleteUchunguzi uliofanywa na taasisi mbali mbali na makundi ya wataalamu Duniani wamethibitisha yakwamba wanandoa ni miongoni mwa watu wanaoishi maisha mengi zaidi kulinganisha na wasio owa au olewa. Vilevile ndoa ni kitu kinachoweza kumuwezesha mtu kuwa na maisha ya furaha na kumuongezea kipato maradufu.kwa kifupi kama mtu anataka kuwa tajiri basi ndoa ni moja ya vitu vinavyoweza kumtimizia ndoto yake hiyo kirahisi. Kama mtu au kijana mambo yake kimaisha hayaendi vizuri basi muarubaini wa tatizo hilo ni kuoa na kuheshimu misingi ya ndoa atashangazwa na mabadiliko atakayoyaona. Sifa ya kuwa wewe ni kidume anauwezo wa kumpata mwanamke yeyote uanaemtaka ni upumbavu mtupu utakaokupelekea majuto mwisho wake. Kasumba kuwa kuoa kunamletea mtu matatizo ni uzaifu wa akili kwani ili mwanadamu apige hatua ya kukua kiakili au kimbinu ni lazima kuwepo na vitu vitakavomfanya afikiri zaidi kuvipatia ufumbuzi ili kumuwezesha kuishi kwa amani zaidi. Mtu yeyote anaeikimbia challenge au vikwazo vya kimaisha badala ya kupambana navyo na kutafuta njia ya mkato ni Coward au muoga na mtu wa aina hiyo siku zote ataendelea kuishi maisha ya ziki. Kuenda kutafuta ngono kwenye bar,au madanguro au Dada powa ni njia ya mkato ya kujitimizia haja ya tendo la ndoa ambapo mtu angeweza kuipata kwa nafasi na usalama zaidi ndani ya ndoa bila kuhofu maambukizo ya maradhi au hata usalama wake wa maisha. Kama kijana anashindwa kuoa kwa kisingizio cha kwamba hana uwezo wakati yupo mtimilifu wa viungo kamili kiafya basi ajue anakasoro kwenye akili yake kwani suala la kijana kupambana na kuwa na sehemu yake ya kuishi na akongezea na ndoa ni kipimo tosha cha mtu kuanza kuyatwala maisha yake na ni moja ya ushindi mtamu katika maisha. Unyonge unaowakabili watu wengi ni kukubali kutawaliwa na maisha na mara nyingi sababu inakuwa ni uzembe na uvivu. Mtu haifai kung'ang'ania sehemu moja tu ya kuishi kama mambo hayaendi vizuri jaribu kubadilisha makazi kwa lengo la kutafuta maisha bora zaidi utafanikiwa tu ila vijana tuwache fikra potofu kuwa kuoa ni kwa ajili ya kutafuta ngono tu peke yake kiukweli ndoa ina faida nyingi sana kwa maisha ya mwanadamu.