Utafiti Waleta Matumaini ya Chanjo ya Virusi vya Corona Kupatikana



Data za awali kutokana na majaribio matatu ya chanjo ya virusi vya corona zinaonyesha imani inayoongezeka kwamba chanjo ya kupambana na virusi hivyo isiyo na madhara makubwa inakaribia kupatikana.

 Iwapo juhudi zinazowekwa zitazaa matunda na kuvumbua chanjo ya kuwakinga mabilioni ya watu kote duniani na kufikisha kikomo janga lililosababisha vifo vya zaidi ya watu laki sita ni jambo ambalo halijabainika.

Chanjo hiyo ambayo inatengenezwa na kampuni ya utengenezaji dawa ya Uingereza AstraZeneca kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Oxford imeonyesha kubuni kwa kinga kwa watu wote waliofanyiwa majaribio ya chanjo hiyo na hakukuonekana madhara yoyote miongoni mwa hao waliojitolea kufanyiwa majaribio.

Chanjo nyengine inayotengenezwa na kampuni ya Cansino Biologics kwa ushirikiano na kitengo cha utafiti cha jeshi la China imeonyesha pia kwamba iko salama na wagonjwa wanakingwa kupata virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad