Utoaji wa Mimba; Uuaji wa kikatili usiokemewa na kupingwa kama inavyostahili
0
July 24, 2020
Ni matumaini yangu kuwa mpo fresh kabisa, mnaendelea na majukumu ya Ujenzi wa taifa letu Tanzania na taifa la Mungu, kwa wale wenye imani hiyo.
Kuna tabia ya, wanandoa na wasio wanandoa, kutoa mimba wakidhani kuwa ni kitendo cha kawaida kabisa. Jambo hilo limechangiwa kwa kiwango kikubwa siku hizi cha Elimu ya Uzazi wa Mpango inayoendelea.
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea watu kuchukua uamuzi huu;
01: Wanafunzi kuhofia kuzuiwa kuendelea na masomo yao.
02: Hali ya maisha kuwa ngumu.
03: Kubakwa
04: Kupata mimba nje ya mipango,
05: Michepuko, n.k.
Sababu zote hizi zinatuma ujumbe mmoja tu; mimba kupatikana bila kutakiwa au kutarajiwa.
Ninawasihi ndugu zangu, tusitoe mimba, tunakuwa wauaji.
Kiumbe, in this case kijusi, kinahesabiwa kuwa hai mara baada ya yai la mama kuungana na mbegu ya baba kutengeza kile ambacho kinaitwa zygote kwa Kiingereza. Mnisamehe sijui Kiswahili chake.
Hivyo; ukiitoa mimba hii kwa njia yoyote, hata kwa kutumia tu vile vidonge vya saa sabini na mbili, unakuwa umeua.
Kwa wanandoa; tutumie njia mbadala za kuepuka mimba kwa kufuata njia ya kalenda na kuepuka kujamiiana siku ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kutunga mimba (kwa wanawake wengi ni siku ya 10-17 ya mzunguko wa hedhi).
Pia, tuwaachie wanandoa tendo hili la ndoa, ukishindwa kabisa, japo sikushauri, basi jamiiana na mtu sahihi ambaye hata ukimpa au akikupa mimba mtakuwa comfortable ama kuoana ama kumlea mtoto huyo, tofauti na hapo;
Jiepushe na tendo la ndoa nje ya ndoa.
Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu, na kwa namna ya pekee Wakatoliki wenzangu; kutoa mimba ni dhambi ya mauaji na kwa Wakatoliki ni dhambi inayoungamwa kwa Mhashamu Baba Askofu pekee, tena inamalipizi makubwa ukilinganisha na dhambi nyingine.
Sote tujiunge pamoja kupigania uhai wa watoto hawa wanaouliwa bila kuwa na uwezo wa wao kujitetea na wasio na hatia.
Ni somo gumu sana, ila ukweli hata kama ni mchungu inabidi tuupokee.
Ninawatakia wakati mwema.
Tags