Waandamanaji Wateketeza Bendera ya Marekani nje ya White House Baada ya Hotuba ya Trump
0
July 05, 2020
Waandamanaji waliokuwa na hasira waliteketeza moto bendera ya Marekani nje ya Ikulu ya White House mjini Washington baada ya hotuba ya Rais Donald Trump kwa mnasaba wa siku ya 'uhuru' wa nchi hiyo jana Julai nne.
Waandamanaji hao wa mrengo wa kushoto walisikika wakisema 'Marekani haijawahi kuwa adhimu' punde baada ya Trump kutoa hotuba yake.
Waandamanaji hao wametaja jinai za Marekani ikiwa ni pamoja na utumwa, mauaji ya kimbari na vita na kisha wakateketeza moto bendera ya Marekani. Moja ya nara kuu za Trump imekuwa ni 'Kuifanya Marekani Adhimu Tena."
Maandamano mengine yalifanyika kote Marekani jana huku waandamanaji wanaopinga ufashisti wakitaka Rais Trump na makamu wake waondolewa madarakani.
Mjini New York waandamanaji wametengeneza na kisha kubomoa sanamu la Rais Trump nje ya 'Jengo la Trump'.
Katika hotuba yake jana Trump aliwashambulia vikali wafuasi wa mrengo wa kulia wakiwemo wakomunisti na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi ambao wamekuwa wakiandamana kupinga mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd.
Tokea mauaji ya Floyd mnamo Mei 25 kumekuwa kukishuhudiwa maandamano mara kwa mara kote Marekani.
Kinachoshuhudiwa sasa nchini Marekani si hasira na vuguvugu la kupita tu la kulalamikia mauaji yaliyofanywa na polisi dhidi ya raia mweusi, George Floyd, aliyegandamizwa na kubinywa shingo na afisa wa polisi hadi kufa katika mji wa Minneapolis, bali ni mlipuko wa hasira za mamia ya miaka ya ukandamiza, dhulma na ubaguzi uliokita mizizi katika jamii ya Marekani dhidi ya watu weusi na jamii za waliowachache.
Tags