Wabunge wa Madagascar Waangamizwa na Corona, Tiba Yao Imeenda Wapi?
0
July 13, 2020
Andry alitangaza kuhusu manaibu wabunge 11 pamoja na maseneta 14 walioambukizwa corona. Picha:Hisani.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina alitangaza Jumapili, Julai 12, kuhusu wabunge wawili walioambukizwa virusi vya corona
Manaibu wabunge wengine 11 pamoja na maseneta 14 pia waliripotiwa kuambukizwa virusi hivyo hatari
Hadi sasa Madagascar ina idadi ya takriban watu 2, 573 walioambukizwa virusi hivyo huku vifo 35 vikiripotiwa
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina alitangaza Jumapili, Julai 12 kuhusu maseneta wawili walioambukizwa virusi vya corona.
Si hao tu , Andry pia alitangaza kuhusu manaibu wabunge 11 pamoja na maseneta 14 walioambukizwa virusi hivyo hatari.
Virusi vya corona vimezidi kuiteketeza nchi hiyo licha ya Rais huyo kujitokeza na kutangaza kuhusu kupatikana dawa ya virusi hivyo nchini humo, nchi nyingi ikiwemo Tanzania ikikimbia kuomba usaidizi wa dawa hiyo kuwatibu wananchi wake.
Rais huyo amekuwa katika mstari wa mbele katika kuzishinikiza mataifa jirani kununua dawa hiyo kutoka kwake.
Dawa hiyo hadi sasa haijathibitishwa na shirika la afya ulimwenguni WHO kuwa dawa inayoweza kutumika katika kutibu wagonjwa wa virusi wa corona.
Madagascar ambayo ilifungua kila eneo la uchumu baada ya kupata dawa ya virusi vya corona ililazimika tena kufunga na kuweka marufuku ya usafiri baada ya idadi ya walioambukizwa virusi hivyo kuongezeka maradufu.
Hadi sasa, nchi ya Madagascar ina idadi ya takriban watu 2, 573 walioambukizwa virusi vya corona na vifo 35.
Wengi sasa wamesalia wakijiuliza swali kuu, je, ikiwa Madagascar ilikuwa na dawa na kutibu corona, ni kwanini dawa hiyo haijawatibu wananchi wake?
Tags