Wabunge Wawili Nchini Madagascar Wamefariki na Virusi vya Corona, 25 Waambukizwa


Wabunge wawili nchini Madagascar wamefariki kutokana na virusi vya corona huku wabunge wengine 25 wakiambukizwa virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kilipothibitishwa katika kisiwa hicho mnamo mwezi Machi , kulingana na rais wa taifa hilo Andry Rajoelina.

Madagascar imeripoti wagonjwa 5,080 waliothibitishwa kuambukizwa tangu wakati huo na vifo 37 kulingana na takwimu za serikali.

Kulinganaa na chombo cha habari cha Reuters hali ya dharura ya kiafya imetangazwa nchini humo tangu mwezi Machi, na mamlaka iliweka amri ya kutotoka nje katika mji mkuu na viungani mwake ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

''Naibu mmoja alifariki. Seneta mmoja pia alifariki. Baada ya kufanyiwa vipimo wabunge 11 walikutwa na corona. Katika bunge la seneti watu 14 wakiwemo maafisa na mawakala wa viongozi hao walipatikana na virusi hivyo'', Rajoelina alisema wakati wa kipindi cha mazungumzo katika runinga siku ya jumapili.

Rajoleina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo ambayo ilizinduliwa mwezi Aprili, licha ya onyo kutoka kwa shirika la Afya duniani kwamba haijaidhinishwa kutumika.

Ni kweli kwamba nimewasiliana na walioambukizwa . Nimeingia katika mahospitali yanayowatibu wagonjwa wa corona. Niko salama'', alisema.

Sina virusi vya corona hata kidogo. Sina dalili. Namshukuru Mungu. Nafuata maagizo niliojiwekea, lakini zaidi ya yote mimi na wapenzi wangu mke wangu na watoto wangu, tunakunywa na kufuata maagizo ya dawa yetu ya mitishamba''

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad