Wabunge wawili waliomaliza muda wao Njombe,wakata rufaa matokeo ya kura za maoni


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Makete Profesa Norman Sigala King Pamoja na Gerson Lwenge Wanging'ombe wamekiandikia barua Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa  Njombe kukata rufaa inayopinga matokeo ya kura za maoni ya Ubunge kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Octoba 28,2020.

Katibu wa siasa,Itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole amewaeleza  wanahabari jana mara baada ya kukamilika  kwa mchakato wa kura za maoni upande wa viti maalum (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa Green City mjini Makambako,Ngole amesema wamezipokea rufaa hizo na watazifanyia kazi kwa kutenda haki kwa kuzingatia taratibu za Chama hicho.

“Hakujawa na malalamiko mengi japo tumepokea rufaa kutoka jimbo la Makete Mh,Norman Sigala amekata rufaa mbunge ambaye alikuwa anamaliza muda wake.Lakini pia tumepokea barua kutoka Wanging’ombe kwa Mh,Gerson Lenge naye inaonyesha hajaridhishwa na kilichotokea na kinachoendelea sasa ni kufuata taratibu za Chama,vipo vikao vinavyosikiliza rufaa” alisema  Erasto Ngole katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe

Vile Ngole amesema mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni kwa upande wa wabunge wa viti maalum kupitia Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) mkoa wa Njombe uliowapa ushindi Mbunge wa viti Maalum aliyemaliza muda wake Bi,Neema Mgaya pamoja na aliyewahi kuwa  Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt,Pindi Hazara Chana kwa kupata kura Neema Mgaya -239,Pindi Chana -202 na Rebecca Nsemwa-151.Huku akifafanua kuwa kinachofuata kwa sasa ni kura za maoni kuwapata madiwani wa kata na viti maalum.

Kwa upande wa kura za maoni jimbo la Makete lililosababisha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Prof,Sigala kukata rufaa,Matokeo ya washindi wa mwanzo yaliwapa ushindi Festo Sanga-116,Norman Sigala-89,Ignatio Mtawa -86 huku wilayani Wanging’ombe Enock Kiswaga-175, Gerson Lwenge-159 na Festo Dugange-92.

Aidha mara baada ya matokeo ya kura za maoni jimbo la Makete,Sigala alinukuliwa na baadhi ya vyombo akifafanua uchaguzi huo kugubikwa na vitendo viovu ikiwemo vitendo vya rushwa.


“Nikawasiliana na TAKUKURU wilaya ya Makete nikampigia simu afisa nikamueleza hali halisi kwamba nimeona mimi na nikamuandikia meseji kwamba hawa watu wanafanya fujo ni vizuri waangaliwe na afisa akaniambia anashughulika na usimamizi ulikuwa haujaanza”amenukuliwa Sigala. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad