Wafahamu Popo Wanaoishi na Virusi vya Corona



WANASAYANSI wanasema wamechunguza vinasaba vya popo sita duniani. Maisha yao yanajumuisha kidokezo cha vinasaba vyao vinavyowafanya kuwa na kinga ya kipekee inayowalinda dhidi ya virusi vya corona.

Watafiti wana matumaini kwamba taarifa hizo zitawasaidia kufahamu siri ya jinsi popo wanabeba virusi vya corona na kuvisambaza bila wao wenyewe kupata maambukizi. Wanasema kuwa huenda hilo likatoa suluhu ya kudumu kusaidia afya ya mwanadamu wakati wa janga hili na hata siku za usoni.

Profesa Emma Teeling kutoka chuo cha Dublin amesema kuwa chembe za urithi walizochunguza zimewafanya kubaini kwamba popo wana mifumo maalum ya kinga. Na kuelewa jinsi popo wanavyoweza kumudu virusi vya corona bila wao kupata maambukizi kunaweza kusaidia kupata tiba mpya ya ugonjwa wa Covid-19.

“Ikiwa tunaweza kuiga kinga ya popo dhidi ya virusi, unaweza kupata tiba, tayari imeshabadilika na kukua, kwa hivyo siyo kwamba uvumbuzi unaanza mwanzo. Sasa tuna vifaa vya kutuwezesha kuelewa hatua tunazohitajika kuchukua; tunahitajika kuvumbua dawa ili kufanikiwa,” amesema  Teeling

Profesa Teeling ni mwanzilishi wa mradi wa Bat1K project, unaopanga kuchunguza vinasaba vya spishi 1,421 za popo walio hai.

“Vinasaba hivi ndivyo vinavyohitajika kubaini suluhu ya kijenetiki inayotokana na popo ambayo hatimaye inaweza kuboreshwa na kuweza kukabiliana na magonjwa,” amesema.

Ugonjwa wa Covid-19 unasemekana kwamba chimbuko lake ni popo ulikosambaa hadi kwa mwanadamu na wao sasa kuanza kusambaziana. Magonjwa mengine pia yakiwemo maradhi ya Sars, Mers na Ebola, pia yanasemekana kwamba yalifika kwa mwanadamu kwa njia hiyohiyo.

Wanaikolojia na wahifadhi wa mazingira wameonya kwamba popo wasiuliwe au kuchukuliwa vibaya; kwa sababu wanapoachwa wakiwa kwenye mahangaiko kwenye mazingira yao wanayoishi huenda wakasababisha hatari kidogo kwa afya ya mwanadamu.

Na pia ni muhimu kwa kuhakikisha urari wa asili duniani. Wengi wao ni wachavushaji, wanatoa mbegu kutoka kwenye matunda na wengine ni wala wadudu ambao hula wadudu tani milioni kadhaa kwa usiku mmoja.

Ni spishi gani ya popo wanaochunguzwa?

Spishi sita za popo: ni popo aina ya horseshoe kwa Kiingereza jamii ya (Rhinolophus ferrumequinum), Egyptian fruit jamii ya (Rousettus aegyptiacus), popo kwa jina pale spear-nosed jamii ya (Phyllostomus discolor), Popo kwa jina greater mouse-eared jamii ya (Myotis myotis), popo Kuhl’s pipistrelle jamii ya (Pipistrellus kuhlii) na popo velvety free-tailed kwa Kiingereza jamii ya (Molossus molossus).

Utafiti umebaini nini?

Timu ya kimataifa ya watafiti inayotumia teknolojia ya kisasa inachunguza chembe za urithi za popo na vinasaba vyao vya sasa. Kwa kulinganisha hilo dhidi ya wanyama wengine wanaonyonyesha 42 waliweza kujua maisha ya popo.

Popo wanaonekana kuwa karibu na kundi la wanyama walao nyama (mbwa na paka na spishi zingine), kakakuona, nyangumi na wanyama wenye kwato. Kukokotoa utofauti wa jenetiki kulibaini chembe za urithi ambazo zimekuwa na mabadiliko tofauti kwa popo jambo ambalo huenda linachangia uwezo wao wa kipekee.

Kazi ya kuchunguza jenetiki zao ilibaini chembe ambazo huenda zinachangia mwangwi wa sauti zao ambayo popo hutumia kuwinda na kutembea kwenye maeneo yenye giza totoro.

Je taarifa hizo zitasaidia vipi kukabiliana na janga hili na mengine ya siku za usoni?

Kazi yao inaathari kwa afya ya mwanadamu na magonjwa kwa kubaini mabadiliko makubwa kwenye chembe za urithi ambayo yanatoa kinga kwa popo dhidi ya virusi.

Watafiti wanafikiria kuwa elimu ya chembe za urithi za popo kutasaidia kuelezea vile wanyama wanaonyonyesha wenye uwezo wa kuruka wanamudu maambukizi ya virusi vya corona, siku za usoni kutasaidia kukabiliana na janga.

“Mabadiliko haya huenda yanachangia popo kuwa na kinga ya kipekee na kuangazia uwezo wao wa kukabiliana na virusi vya corona,” amesema Dkt. Michael Hiller wa Taasisi ya Max Planck ya masuala ya Biolojia na Jenetiki huko Dresden, Ujerumani.

Katika maambukizi mengi yanayosambaa, siyo virusi pekee vinavyochangia kifo, lakini pia uvimbe mkubwa unakotokana na mfumo wa kinga ya mwili. Popo wanaweza kudhibiti hili. Kwa hiyo, ingawa pengine huenda wanaweza kupata maambukizi, hawaoneshi dalili za ugonjwa wenyewe.

Utafiti huu umechapishwa kwenye jarida la Nature.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad